Dodoma FM

Sheria yawalinda watoa taarifa za rushwa

28 January 2026, 1:10 pm

Picha ni Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba katika  Hafla ya Ufunguzi wa Mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU, uliofanyika Cate Hotels Morogoro. Picha na takukuru.tz.

Malecha amehitimisha kwa kusema kuwa ili kukabiliana na vitendo vya rushwa TAKUKURU imeendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na kutoa elimu shuleni kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu , huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa ili kujenga jamii yenye haki, uwazi na maendeleo.

Na Anwary Shabani.

Imeelezwa kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Sheria namba 11 ya mwaka 2007, kila mwananchi nchini anatakiwa kutoa taarifa pindi anapoona vitendo vya rushwa vinatendeka au vinapokaribia kutendeka katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza na Taswira ya Habari, Faustine Malecha, ambaye ni Mkuu wa Uelimishaji wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, amesema kuwa mapambano dhidi ya rushwa si jukumu la TAKUKURU pekee bali ni wajibu wa kila mwananchi kwa mujibu wa sheria.

Sauti ya Faustine Malecha.

Malecha ameongeza kuwa kulingana na kifungu cha 57 na 58 cha sheria  namba 11 ya mwaka 2007 kinamlinda mwananchi anayetoa taarifa za rushwa, hivyo wananchi hawapaswi kuogopa kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapogundua au kuona viashiria vya rushwa.

Sauti ya Faustine Malecha.

Taswira ya habari imepita  wa Mtaa wa Mwatano uliopo kata ya Miyuji jijini Dodoma na kuzungumza na baadhi ya wananchi, ambapo wananchi hao wamebainisha kuwa miongoni mwa changamoto inayowafanya wasitoe taarifa za rushwa kwa mamlaka husika ni ukosefu wa elimu.

Sauti za wananchi.