Dodoma FM

Vijana wahimizwa kujiunga na VETA na kuachana na mitazamo hasi

21 January 2026, 2:40 pm

Picha ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA CPA Antony Kasore akiongea katika mkutano na waandishi wa habari. Picha na Dodoma FM.

Mnamo mwaka 2016 takwimu za Umoja wa Mataifa zilionesha kuwa uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia 7 lakini licha ya mafanikio haya, ukosefu wa ajira miongoi mwa vijana bado ni changamoto kubwa ikiwa katika kiwango cha asilimia 12.

Na Anwary Shabani.

Jamii imetakiwa kuachana na mitazamo hasi kuhusu kuwapeleka vijana katika vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) ili kuondokana na changamoto ya ajira ambayo imekuwa ikiwakabili vijana wengi nchini.

Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa mataifa inaelezwa kuwa kwa kila vijana 700,000 ambao wanasaka ajira kila mwaka ni fursa 40,000 tu ambazo ziko wazi hii ikimaanisha kwamba ni asilimia 6 tu ya vijana ambao wanapata kazi rasmi.

Taswira ya habari imewatembelea vijana ambao wamehitimu chuo cha ufundi stadi Veta na kupata mafunzo mbalimbali hapa wanaeleza jinsi mafunzo hayo yalivyo wasaidia wao kujiajiri na kujiingizia kipato cha kila siku.

Sauti za vijana.
Picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati wa kikao kazi cha kimkakati kati ya Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara jijini Dodoma. Picha na Wizara ya Eimu.

Hivi karibuni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Profesa Adolf Mkenda, amesema Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia elimu ya ujuzi.

Dkt. Omar alisema serikali imeendelea kuwekeza katika vyuo vya VETA, kuongeza miundombinu na kuboresha mitaala ili iendane na mahitaji ya soko la ajira.

Sauti ya Hussein Omar.

Serikali na wadau wa elimu wanaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwahamasisha vijana kujiunga na vyuo vya ufundi stadi, kama njia mbadala ya kukabiliana na tatizo la ajira nchini.