Dodoma FM
Dodoma FM
20 January 2026, 6:03 pm

kumekuwa na ushirikiano wa karibu baina ya wawekezaji na wananchi hivyo imekuwa rahisi wananchi kunufaika na misaada kutoka Kwa wawekezaji hao.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kijiji cha Nayu Kata ya Dabalo Wilayani Chamwino wametoa pongezi Kwa wawekezaji wa migodi ya dhahabu katika Kijiji Chao Kwa misaada ya kijamii wanayo itoa.
Wakizungumza na Taswira ya habari miongoni mwa wakazi hao wamesema misaada hiyo ya kijamii ambayo inatolewa na wawekezaji hao inawasaidia wananchi na kuwapa matumaini ya kupiga hatua za maendeleo.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Nayu Bw.Samsoni Noha amesema kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu baina ya wawekezaji na wananchi hivyo imekuwa rahisi wananchi kunufaika na misaada kutoka Kwa wawekezaji hao.
Noha ameongeza kuwa kupitia uwekezaji wa sekta ya madini wamefanikiwa kutoa misaada ya chakula mashuleni sambamba na usimamizi wa ofisi za kijiji pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo .