Dodoma FM
Dodoma FM
16 January 2026, 3:27 pm

Besiimire amesema duka hilo ni mkombozi kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani iliyo katika Kanda ya Kati kutokana na kuboreshwa kwa huduma zake.
Na Yussuph Hassan.
Kampuni ya Mtandao wa Simu ya Vodacom imesema imejipanga kuhakikisha inatoa huduma yenye kipaumbele kwa makundi maalumu kwa kuwasimamia nakuwapa huduma bora sawa na wateja wengine.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kanda ya kati Vodacom Chiha Nchimbi na Msimamizi wa Maduka ya Vodacom Kanda ya Kati Bernard Kombe , wakati wa Uzinduzi wa Duka la Vodacom Jijini Dodoma ambapo wamesema watahakikisha makundi ya watu wenye mahitaji maalumu wanahudumiwa kwa wakati na kujali hali Zao.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire amesema watahakikisha wanaboresha Huduma na kukuza mawasiliano Maeneo mengi zaidi.