Dodoma FM
Dodoma FM
15 January 2026, 2:20 pm

Wananchi hao wamefurahishwa na ujio wa mradi huo, huku wakiongeza kuwa mradi huo utawapunguzia umbali ambao walikuwa wakitembea kutafutamaji safi na salama.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kijiji cha Msanga Wilayani Chamwino wameipongeza Serikali Kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji kijijini hapo.
Wakiongea na taswira ya habari wanasema ujio wa mradi wa maji kijijini hapo utamaliza adha ya maji ambapo hapo awali walilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Msanga Bw.Tibu Ally amesema kukamilika Kwa mradi wa maji Kijiji hapo utasaidia kutibu changamoto ya maji katika vitongoji vingi vya Kijiji hicho