Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuhakikisha watoto wanaripoti shuleni mapema

13 January 2026, 4:36 pm

Picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe akiwa pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoma, na mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini wakati wakikagua miuondombinu ya shule.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dodoma mh. Rosemery Senyamule Idadi ya Wanafunzi wanaotarajiwa kuanza Muhula Mpya wa Masomo 2026 ulio anza leo kwa elimu ya awali ni 79, 131, darasa la kwanza kwa shule za msingi ni wanafunzi 82,569 huku kidato cha kwanza kwa upande wa sekondari ni wananfunzi 46,453.

Na Mariam Kasawa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe ametoa wito kwa wazazi na walezi kote nchini kuhakikisha wanawandikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule katika shule za msingi na sekondari kwa wakati, akisisitiza kuwa elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto.

Waziri amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu, ikiwemo ujenzi wa madarasa, upatikanaji wa walimu pamoja na mazingira rafiki ya kujifunzia, hivyo hakuna sababu kwa mtoto yeyote kukosa fursa ya elimu.

Sauti ya Prof Riziki Shemdoe .

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma mh Rosemery Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma umejipanga vizuri na maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa darasa la awali na msingi, kuanza Muhula mpya wa masomo 2026.

Sauti ya Mh.Rosemery Senyamule .