Dodoma FM

Ukosefu wa maji safi waibua hofu Matembwe

13 January 2026, 1:50 pm

Picha ni ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma. Picha na DUWASA.

Wakazi hao wamekumbwa na hofu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwani maji ya mvua yanayotiririka kutoka maeneo mbalimbali yanachanganyika na maji ya mto huo, hali inayoleta hofu ya matumizi ya maji yasiyo safi na salama.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa Matembwe wilayani Chamwino jijini Dodoma wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na maji ya mto wanayotumia kutokuwa safi na salama.

Wakizungumza na taswira ya habari  wamesema ukosefu wa maji safi na salama umepelekea wanawake wa eneo hilo kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji hali inayokwamisha shughuli zingine.

Sauti za wananchi.

Anania Ngodingo mwenyekiti wa vitongoji hivyo amekiri uwepo wa matumizi ya maji ambayo ni hatari kwa afya za wananchi kutokana na mchanganyiko wa shughuli za uchimbaji madini mlimani ambalo ndipo chanzo cha maji hayo.

Sauti ya Anania Ngodingo.