Dodoma FM
Dodoma FM
9 January 2026, 3:52 pm

Kikao hicho kimelenga kutoa elimu ya awali na kujenga uelewa kwa viongozi kuhusu mpango huo muhimu kwa ustawi wa wananchi.
Na Kitana Hamis.
Wilaya ya Kiteto imeonyesha utayari mkubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote baada ya kufanyika kwa kikao maalum cha Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) ngazi ya Wilaya ameyasema hayo Januari, 2026 mjini Kibaya.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema amesema mpango huo ni sehemu ya ahadi ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya bila kikwazo na kwa gharama nafuu. Ameongeza kuwa Wilaya itaendelea kutoa elimu kupitia mikutano ya tarafa na vijiji vyote.

Viongozi wa Wilaya na Halmashauri wameahidi kushirikiana kuhakikisha wananchi wote wa Kiteto wanapata taarifa sahihi na uelewa wa kina kuhusu mpango huu wa kitaifa.