Dodoma FM

Wazazi, walezi wahimizwa kusaidia mabadiliko ya tabia kwa vijana

8 January 2026, 4:25 pm

Mtaalam wa Saikolojia ya jamii kutoka shirika la KISEDETI jijini Dodoma. Picha na Noah Patrick.

Akihitimisha, Mtahu amebainisha mikakati ya KISEDETI ikiwemo kuendelea kuandaa programu za malezi salama, kuwatambua na kuwafuatilia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani pamoja na kuanzisha mashamba darasa, hatua zinazolenga kupunguza idadi ya watoto na vijana wanaoishi na kufanya kazi mitaani na kuwajengea maisha bora ya baadaye.

Na Lilian Leopold.

Wazazi na walezi jijini Dodoma wamehimizwa kutoa ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko chanya ya tabia kwa vijana waraibu pamoja na wale wanaoishi na kufanya kazi mitaani, ili kupunguza ongezeko la kundi hilo katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, Mtahu Mtahu, wakatiakizungumza na Dodoma FM kutoka shirika lisilo la kiserikali la KISEDETI linalojishughulisha na kusaidia watoto na vijana wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Mtahu amesema kuwa KISEDETI imejikita katika kuwasaidia watoto na vijana wanaotoka katika mazingira magumu kwa kuwapatia msaada wa kisaikolojia, elimu ya malezi salama pamoja na kuwaandaa kuishi maisha yenye mwelekeo chanya ndani ya jamii.

Sauti ya Mtahu Mtahu.

Ameeleza kuwa jamii ina nafasi kubwa katika kufanikisha mabadiliko ya tabia kwa vijana hao, akisisitiza umuhimu wa kuwapokea, kuwaheshimu na kuwasaidia vijana wanaoishi na kufanya kazi mitaani badala ya kuwanyanyapaa.

Aidha, Mtahu ameongeza kuwa shirika hilo limekuwa likitoa elimu kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhusu malezi salama, ikiwa ni njia ya kuwajengea wazazi uelewa wa namna bora ya kushughulikia watoto na vijana wanaopitia mabadiliko ya kitabia.

Sauti ya Mtahu Mtahu.