Dodoma FM
Dodoma FM
5 January 2026, 5:25 pm

Aidha, uongozi unahamasisha usafi wa pamoja, kudhibiti maeneo yanayozalisha mbu, na kushirikiana na wataalam wa afya ili kuzuia milipuko ya magonjwa, huku wakisisitiza umuhimu wa kushirikiana kwa jamii ili kulinda afya zao na za familia zao.
Na Anwary Shabani.
Jamii imetakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za kiafya ikiwemo kuchemsha maji ya kunywa na kunawa mikono kwa kutumia maji safi nayanayotiririkaili kujikinga na magonjwa ya mlipuko, hasa katika kipindi hiki cha mvua.
Hayo yameelezwa wakati Taswira ya Habari ilipotembelea mtaa wa Mwatano, uliopo kata ya Miyuji jijini Dodoma, ambapo wamezungumza na baadhi ya wananchi kuhusu namna wanavyokabiliana na magonjwa ya mlipuko hususani wakati huu wa mvua.
Wananchi wa mtaa huo wamesema kuwa wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali za kujilinda ikiwemo kuchemsha maji ya kunywa, kutumiavyoosafi, kutega chandarua pamoja na kuchoma dawa za kuua mbu, hatua ambazo zinalenga kupunguza maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na malaria.
Kwa upande wake, Katibu wa Shina wa Mtaa wa Mwatano, Aderiki Fredrick, amesema kuwa uongozi wa mtaa huo unaendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kuhamasisha usafi wa mazingira, ikiwemo kufanya usafi wa pamoja na kuhakikisha maeneo yanayozalisha mbu yanadhibitiwa ili kuzuia milipuko ya magonjwa.
Wananchi wametakiwa kuendelea kushirikiana na viongozi wa mitaa pamoja na wataalamu wa afya kwa kuzingatia kanuni za usafi ili kujilinda wao na familia zao katika kipindi hiki cha mvua.