Dodoma FM
Dodoma FM
23 December 2025, 3:47 pm

Katika semina hiyo, waandishi wa habari walifahamishwa kuwa Serikali inaruhusiwa kununua bidhaa tatu pekee zilizotumika kwa manufaa ya umma,treni,meli na ndege.
Na Mariam Kasawa.
Meneja Mafunzo wa Mamlaka ya PPRA, Gilbert Kamnde, amewafafanulia waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika semina maalum ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu PPRA na majukumu yake.
Kamnde amesema kuwa utendaji wa PPRA umeainishwa na Bunge mwaka 2001 pamoja na Kanuni za GN Namba 518 za mwaka 2024, ambazo zinatoa mwongozo wa utekelezaji wa majukumu ya ununuzi wa umma. Aidha, ameeleza namna mfumo wa NeST unavyotumika katika kusimamia na kurahisisha taratibu za manunuzi ya umma.