Dodoma FM

Uhaba wa matundu ya vyoo wahatarisha afya za wanafunzi Mlebe

22 December 2025, 3:54 pm

Matundu manne yaliyopo yaliyopo shuleni hapo yanahudumia wanafunzi zaidi ya 700 hali ambayo ni hatari.Picha na habari leo.

Aineya ameongeza kuwa wanafikilia kuwashirikisha wananchi katika mkutano  wa hadhara wa mwezi huu wa kumi na mbili Ili kuona namna ya kuanza mchakato wa kutafuta fedha za ujenzi wa vyoo vingine.

Na Victor Chigwada.
Uhaba wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mlebe Kata ya Msamalo Wilaya ya Chamwino umekuwa kikwazo kwa wanafunzi hao hali inayopelekea hatari ya kuibuka kwa agonjwa ya mlipuko.
Baadhi ya wanafunzi wakizungumzia changamoto hiyo wameeleza kuwa matundu manne yaliyopo hayajitoshelezi kuwahudumia hivyo imekuwa hatari Kwa matumizi pia vyoo hivyo ni vya muda mrefu .

Nao baadhi ya wazazi wa Mlebe wameiomba Serikali kutatua changamoto hiyo kwa wanafunzi kwani idadi ya matundu ya vyoo iliyopo haikidhi mahitaji ya wanafunzi kwani matundu manne ya vyoo wanatumia zaidi ya wanafunzi 700.

Naye mtendaji wa Kijiji Cha Mlebe Bw.simoni Aineya amesema kuwa changamoto kubwa katika sekta ya elimu kijijini hapo ni upungufu wa miundombinu ya madarasa, madawati sambamba na matundu ya vyoo

Aineya ameongeza kuwa wanafikilia kuwashirikisha wananchi katika mkutano wa hadhara wa mwezi huu wa kumi na mbili Ili kuona namna ya kuanza mchakato wa kutafuta fedha za ujenzi wa vyoo vingine.