Dodoma FM

Serikali kuhakikisha watoto wanao ishi katika mazingira magumu wanafikiwa

19 December 2025, 3:14 pm

Picha na Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Nandera Mhando.Picha na Maendeleo ya jamii.

Serikali ilichukua hatua ya haraka ya kufuatilia hali ya mtoto huyo baada ya kupata taarifa hizo kwa kumtafuta Bibi wa mtoto huyo katika hospitali ya Agha Khan jijini Dodoma.

Na Mariam Matundu.

Serikali imeendelea kusimamia na kuhakikisha kwamba watoto wote nchini hususani wanaoishi katika mazingira magumu wanafikiwa na kupatiwa huduma stahiki.

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Nandera Mhando alipofika kusikiliza mashauri ya mtoto aliyeripotiwa katika mtandao wa kijamii (jambo tv)kuishi katika mazingira magumu akiwa chini ya uangalizi wa bibi yake  Desemba 18, 2025 jijini Dodoma.

Dkt. Nandera ameeleza kwamba Serikali ilichukua hatua ya haraka ya kufuatilia hali ya mtoto huyo baada ya kupata taarifa hizo kwa kumtafuta Bibi wa mtoto huyo katika hospitali ya Agha Khan jijini Dodoma.

Awali akizungumza Afisa Ustawi wa jijini Dodoma Rachel Balisidya amesema familia ya Bibi huyo haikua na changamoto za kufikia hatua ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari kwani watoto wake wanamhudumia na kushirikiana nae hatua kwa hatua..

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Nghongona Leah Mwagama amesema baada ya kusikiliza kwa umakini yaliyozungumzwa na Kamishna wa Ustawi, Bibi wa Mtoto huyo ameridhia kuikabidhi Serikali mtoto huyo ili aweze kupata lishe bora mpaka atapofikia miaka miwili.

Habari ustawi.