Dodoma FM

Vijana watakiwa kuwekeza katika kilimo

19 December 2025, 2:56 pm

Vijana wanapaswa kushiriki katika ujasiriamali na ubunifu kwenye sekta ya kilimo .Picha na DW.

Ripoti ya Youth in Agriculture Strategy 2016-2021 inaonesha kuwa vijana wengi hukumbana na changamoto za ardhi, mtaji, teknolojia na mitazamo hasi kuhusu kilimo huku Serikali kupitia Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) inalenga kuwasaidia vijana kuingia kwenye kilimo biashara hali itakayo Saidia kuondoa wimbi la ukosefu wa ajira nchini.

Wito umetolewa kwa vijana nchini kuwekeza nguvu kwenye kilimo nakuachana na dhana ya ukosefu wa ajira hali itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, zaidi ya 70% ya Watanzania ni vijana chini ya miaka 35 Lakini ni takribani 12% tu ya vijana ndio wanaojihusisha moja kwa moja na kilimo.

Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya vijana kujua mitazamo yao juu ya kujihusisha na kilimo wamekiri kuwa ajira ni chache duniani kote na endapo watakuwa na mitazamo Chanya kuhusu kilimo ni rahisi kujikwamua kiuchumi.

Sauti za vijana,

Hassan Kisetto ni Afisa kilimo halmashauri ya mji Kondoa ameiambia Taswira ya Habari kuwa mkakati wa serikali hivi sasa nikuhakikisha wanahamasisha Pamoja na kuwezesha vijana kujiunga na kilimo kupitia vikundi huku vikundi hivyo vikitoa hamasa kwa wenzao.

Sauti ya Hassan Kisetto .