Dodoma FM
Dodoma FM
18 December 2025, 4:29 pm

Mhe Senyamule amesema halmashauri zote na mkoa kwa ujumla kiwango kwa ufaulu Dodoma kimepanda.
Na Yussuph Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa shime kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wadau wengine katika sekta ya elimu kuendelea kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya shule kwa ajili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza January, 2026.
Ni mara baada ya kukagua Miradi ya majengo ya Shule za Msalato Girls’ na Iyumbu Sekondari ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kuanza masomo mwezi January, 2026, Ziara hiyo imefanyika Desemba 17/2025 Jijini hapa.
Mhe Senyamule amesema halmashauri zote na mkoa kwa ujumla kiwango kwa ufaulu Dodoma kimepanda hivyo kwa wanafunzi wote wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani lazima waanze masomo January 2025.