Dodoma FM
Dodoma FM
10 December 2025, 3:53 pm

Ili kupunguza athari zitokanazo na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wameshauri ni vyema elimu ikaotolewa ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza. Picha na Mtandao.
Asilimia 95% ya vijana wenye umri wa miaka 13–17 hutumia mitandao ya kijamii kama TikTok, Instagram, Facebook huku tafiti zinaonesha kuwa vijana wanaotumia mitandao zaidi ya saa 3 kwa siku wako kwenye hatari kubwa ya kupata matatizo ya afya ya akili kama msongo wa mawazo, huzuni, na wasiwasi.
Na Benard Komba.
Baadhi ya vijana Jijini Dodoma wamekiri kukithiri kwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii huku wakidai hali hiyo inaweza kupelekea wimbi kubwa la vijana wenye msongo wa Mawazo.
Juma Kisoko Pamoja na Given Mkolo wameiambia taswira ya Habari kuwa kitendo cha kukuwa kwa utandawazi kwa kiwango kikubwa imekuwa mzigo mkubwa kwa vijana huku wakushindwa kuhimili.
Peter Njau ni mtaalamu wa saikolojia amekiri kuwepo kwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa vijana huku wengine wakitumia muda mwingi hali inayopelekea kuathiri shughuli za kijamii na baadaye kupelekea matatitizo ya afya ya akili.
Aidha ameitaka jamii kuchukua hatua stahiki pindi wanapogundua vijana wao kuwa na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.