Dodoma FM
Dodoma FM
4 December 2025, 1:20 pm

Vijana wenye umri wa miaka 15–24 bado wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huku vijana wa kike wakichangia takribani asilimia 80 ya maambukizi mapya. Picha na Mtandao.
Miongoni mwa sababu nyingine ambayo inaelezwa ni pamoja na vijana wengi kujihusisha katika mazingira hatarishi.
Na Benard Komba.
Serikali imeombwa kuwekeza nguvu kubwa ya utoaji wa elimu ikiwemo kutumia mabango kwenye maeneo ya uma kuhusu virusi vya ukimwi lengo ikiwa kupunguza kasi ya maambukizi mapya hususani kwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24.
Baadhi ya vijana wameiambia taswira ya Habari kuwa ukosefu wa elimu ya maambukizi na namna ya kujikinga na virusi vya ukimwi ndio chanzo kikuu.
Aidha vijana hao wameshauri kuwa njia sahihi ya kujilinda na kupunguza kasi ya maambukizi mapya nikuwa na mpenzi mmoja Pamoja na kutumia kinga kama wataalamu wa afya wanavyoelekeza.
Disemba mosi ya kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya ukimwi duniani Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), William Lukuvi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam alinukuliwa akisema vijana wenye umri wa miaka 15–24 bado wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huku vijana wa kike wakichangia takribani asilimia 80 ya maambukizi mapya.