Dodoma FM

Wasichana waongoza maambukizi ya VVU

2 December 2025, 12:48 pm

Picha ni ‎Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) William Lukuvi, katika Madhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani. Picha na Jambo Tv.

Hapo jana Desemba 1,2025 katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Serikali imesema inaendelea kuwekeza katika huduma za kinga na elimu kuhusu VVU, kwa kuangazia zaidi kundi la vijana.

Na Yussuph Hassan.

Makundi rika na kukosa msimamo wa muda sahihi wa kuwa kwenye mahusiano kwa baadhi ya vijana  zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu za kundi la wasichana kuongoza kupata maambukizi mapya.

Hapo jana wakati dunia ikiadhimisha siku ya ukimwi duniani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), William Lukuvi, amesema vijana wenye umri wa miaka 15-24 bado wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huku vijana wa kike wakichangia takribani asilimia 80 ya maambukizi mapya.

Francis Mbwilo kutoka chama cha uzazi na malezi Tanzania (Uumati) anasema kuwa wasichana wengi wanakosa msimamo kwenye mahusiano kutokana na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu waliowazidi kila kitu.

Sauti ya Francis Mbwilo.

Aidha Dkt Francis ameelezea namna mihemko kwa vijana wa kike inavyoweza kusababisha kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Sauti ya Francis Mbwilo.

Kwa upande wao baadhi ya vijana wamesema wamekuwa wakipatiwa elimu ya afya ya uzazi lakini mihemko imekuwa ikisababisha kushindwa kuchukuwa tahadhari dhidi ya VVU.

Sauti za vijana.

Aidha Serikali inatekeleza elimu ya VVU na Ukimwi, upimaji wa hiari, pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana waliopo shule, vyuoni na wale waliopo nje ya taasisi za elimu ili kupunguza maambukizi mapya.