Dodoma FM

Bodaboda si njia ya mkato kwa kila kijana kufanikiwa

26 November 2025, 2:04 pm

Ingawa kazi ya bodaboda inawaingizia kipato, si kazi ya kudumu ambayo kila kijana anapaswa kuitegemea.Picha na mtandao.

Hata hivyo, sekta hii inakabiliwa na changamoto za usalama, ushindani, gharama za uendeshaji na mahitaji ya kisheria.

Na Mariam Kasawa.
Vijana wametakiwa kujituma katika shughuli mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi na kuacha kuamini kwamba kazi ya bodaboda ni suluhisho pekee kwa kila kijana aliyeshindwa kusoma.

Baadhi ya Vijana wa mtaa wa Jamaica wanaojishughulisha na kazi hiyo wakizungumza na Dodoma fm, wamekiri kuwa licha ya changamoto nyingi, kazi ya bodaboda imekuwa mkombozi kwao kwani inawasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku pamoja na familia zao.

Sauti ya Baadhi ya Vijana wa mtaa wa Jamaica

Kama ilivyo desturi ya makundi mengine, vijana hawa wameunda kikundi cha umoja kinachowajumuisha katika shida na raha. Mwenyekiti wa kijiwe cha Jamaica, Bw. Amon Makuya, amesema ingawa kazi ya bodaboda inawaingizia kipato, si kazi ya kudumu ambayo kila kijana anapaswa kuitegemea.

Sauti ya Bw. Amon Makuya.

Biashara ya bodaboda imekuwa mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi katika nchi zinazoendelea, ikichangia ajira na kurahisisha usafiri wa jamii.