Dodoma FM

Udogo wa Tenki wapelekea adha ya maji Mzula

26 November 2025, 1:44 pm

Tenki hilo limekuwa likishindwa kuhudumia wakazi wote, hali inayowalazimu kutafuta maji kwenye visima, makorongo na mabwawa.Picha na mtandao.

Wameeleza kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi akina mama na kuhatarisha afya za jamii.

Na Victor Chigwada.
Maji ni uhai, lakini wakazi wa Kijiji cha Mzula, kata ya Muungano, Wilaya ya Chamwino, bado wanakabiliana na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kutokana na udogo wa tenki lililopo.

Wananchi wamesema tenki hilo limekuwa likishindwa kuhudumia wakazi wote, hali inayowalazimu kutafuta maji kwenye visima, makorongo na mabwawa.

Wameeleza kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi akina mama na kuhatarisha afya za jamii.

Sauti za wananchi.

Hali inaenda tofauti na Sera ya Taifa ya Maji ya 2025, iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, inasisitiza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote, kulinda vyanzo vya maji, na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya maji.

Aidha Serikali imeweka mkazo katika kusimamia miradi ya maji ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi wengi zaidi, sambamba na kuimarisha miundombinu ya maji vijijini na mijini.

Kwa Upande wa serikali ya kijiji cha Mzula kupitia Kenneth Msanjila, amekiri kuwa tenki lililopo halikidhi mahitaji ya sasa kwa kuwa lilijengwa kutokana na idadi ndogo ya wananchi waliokuwepo wakati huo.

Sauti ya Kenneth Msanjila.