Dodoma FM

Vijana watakiwa kushiriki mikutano ya mtaa

25 November 2025, 2:19 pm

Mikutano ya serikali za mitaa imekuwa ikitumika kujadili masuala muhimu ya maendeleo ikiwemo elimu, afya, barabara na ulinzi.Picha na AI.

Ni wajibu wa vijana kuhudhuria mikutano ya mtaa ili kupata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo.

Na Lilian Leopold.
Vijana wametakiwa kuongeza ushiriki wao katika mikutano ya mtaa ili kufahamu fursa zilizopo kwenye jamii na kupata nafasi ya kuwasilisha changamoto zinazowahusu moja kwa moja.

Mikutano ya serikali za mitaa imekuwa ikitumika kujadili masuala muhimu ya maendeleo ikiwemo elimu, afya, barabara na ulinzi na jinsi ya kutatua changamoto hizo kwa kushirikiana na wananchi.

Akizungumza na Taswira ya habari Meneja Miradi kutoka Taasisi ya Vijana Makao Makuu ya Dodoma Charles Ruben, amesema ni wajibu wa vijana kuhudhuria mikutano ya mtaa ili kupata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo.

Sauti ya Charles Ruben.

Aidha Charles amewataka vijana kubadili mitazamo potofu kuwa mikutano ya mtaa ni kwa ajili ya wazee pekee.

Sauti ya Charles Ruben.

Kwa upande wao baadhi ya vijana kutoka mtaa wa Mathias jijini Dodoma majukumu yao ya kila siku yamekuwa yakichocheo kutoshiriki mikutano hiyo, licha ya kutambua umuhimu wake.

Sauti za vijana.