Dodoma FM

Umbali mrefu wa shule changamoto kwa wanafunzi mtaa wa Matias

25 November 2025, 8:23 am

Wananchi wa mtaa huo wamesema wanahitaji suluhisho la haraka ili kuinusuru elimu ya watoto wao.Picha na AI.

Mwenyekiti wa mtaa huo Bi Dorini amewaomba wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kushirikiana na serikali za mitaa katika kufanikisha ujenzi wa shule hiyo.

Na Anwary Shaban.
Wananchi wa Mtaa wa Matiasi jijini Dodoma wameeleza kuendelea kutaabika kutokana na changamoto ya ukosefu wa shule za msingi na sekondari, hali inayowalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu kila siku ili kufuata shule zilipo.

Taswira ya Habari imefika katika mtaa huo na kujionea hali halisi ya watoto wakisafiri kwa miguu, jambo linalowaweka kwenye hatari na kuwaletea uchovu mwingi.

Sauti za wananchi.

Wananchi hao wamesema wanahitaji suluhisho la haraka ili kuinusuru elimu ya watoto wao, wakisisitiza umuhimu wa serikali kujenga shule ndani ya Mtaa wa Matiasi.

Sauti za wananchi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Matiasi, Dorini Deogratias, amethibitisha kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza hatua zinazochukuliwa.

Sauti ya Dorini Deogratias.

Kwa mujibu wa Sera ya Elimu na Mpango wa Serikali Kwa mujibu wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, serikali inalenga kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora kwa kusogeza huduma karibu na wananchi, ikiwemo ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Sera hiyo inasisitiza kupunguza umbali wa wanafunzi kufuata shule na kuhakikisha mazingira rafiki ya kujifunzia.

Aidha, kupitia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP), serikali imeweka mkakati wa kujenga shule mpya na kuboresha miundombinu ya zilizopo, hususan katika maeneo ya mijini yanayokua kwa kasi kama Dodoma.

Mpango huo unalenga kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuhakikisha kila kata au mtaa unakuwa na shule ya msingi na sekondari.