Dodoma FM
Dodoma FM
21 November 2025, 2:03 pm

Naye, Meneja wa TANROADS Dodoma, Mhandisi Zuhura Amani, amesema wataendelea kufuatilia na kuwasisitiza wakandarasi wote kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa mujibu wa mkataba.
Na Seleman Kodima.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameagiza kukamatwa kwa wakandarasi wa kampuni ya China First Highway Engineering Co. Ltd. kwa kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba wa ujenzi wa barabara licha ya serikali kulipa sehemu ya malipo.
Kampuni hiyo ilipewa jukumu la kujenga barabara ya Ntyuka–Mvumi Hospitali–Kikombo yenye urefu wa kilomita 53, na tayari imelipwa shilingi bilioni 9.68 sawa na asilimia 10 ya malipo, lakini utekelezaji umefikia asilimia 2 pekee badala ya 13 iliyotarajiwa.
Ulega ameagiza Jeshi la Polisi na TAKUKURU kumshikilia na kumuhoji mkandarasi huyo, huku akisisitiza kuwa serikali haitavumilia wakandarasi wasio na uwezo wa kukamilisha miradi kwa wakati.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, amesema watafanyia kazi maelekezo hayo haraka ili kutatua changamoto za miradi inayosuasua.