Dodoma FM
Dodoma FM
19 November 2025, 3:50 pm

Hata hivyo, wapiga picha hao wameeleza kuwa wanakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kutolewa maneno ya kashfa na baadhi ya wateja pindi wanapojaribu kuonesha ubunifu wao kwa lengo la kuwashawishi kupata huduma.
Na Farashuu Abdallah.
Katika jitihada za kupambana na changamoto ya ajira nchini, baadhi ya vijana wa jiji la Dodoma wameamua kujiajiri kupitia fani ya upigaji wa picha mnato.
Wakizungumza na Dodoma FM, vijana hao kutoka eneo la Nyerere Square wamesema kuwa kazi ya upigaji picha imekuwa nguzo muhimu kwao kwani inawawezesha kuendesha maisha ya kila siku. Aidha, wamewashauri vijana wenzao kuchangamkia fursa kama hii ili kujipatia kipato halali na kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wao, wakazi wa eneo la Nyerere Square wamewasihi wananchi wa Dodoma na mikoa mingine kutembelea eneo hilo, wakieleza kuwa mbali na kupata huduma ya picha, Nyerere Square ni sehemu tulivu yenye mandhari ya kuvutia.