Dodoma FM
Dodoma FM
12 November 2025, 1:32 pm

Hata hivyo, Meena amewataka wananchi kuzingatia ushauri na maelekezo ya madaktari kabla ya kutumia dawa, ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika.
Na Lilian Leopold.
Wataalamu wa afya wameonya kuhusu matumizi ya dawa sambamba na maziwa au bidhaa zinazotokana na maziwa, wakisema hali hiyo inaweza kupunguza ufanisi wa dawa mwilini na kusababisha ugonjwa kudumu kwa muda mrefu.
Amani Meena, mwanafunzi wa Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, amesema maziwa yana madini yanayoathiri utendaji kazi wa dawa mwilini.
Akizungumza na Taswira ya Habari, Meena ameeleza kuwa mwingiliano huo unaweza pia kusababisha kichefuchefu kwa baadhi ya wagonjwa.
Kwa mujibu wa baadhi ya wananchi kutoka eneo la Mipango jijini Dodoma, wamesema sababu kubwa ya watu kutumia dawa pamoja na maziwa ni kutaka kupunguza ukali wa dawa.