Dodoma FM

Mnoko yaiomba serikali kuwasogezea huduma ya umeme

7 November 2025, 3:50 pm

Kukosekana kwa umeme kunarudusha nyuma maendeleo ya kitongoji hicho.Picha na REA.

zaidi ya vitongoji 7 kati ya 10 katika Kijiji cha Mpwayungu vina uhitaji na nishati ya umeme

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa kitongoji cha Mnoho Kijiji Cha Mpwayungu jijini Dodoma wameiomba serikali kuwapelekea huduma ya nishati ya umeme itakayosaidia katika shughuli mbalimbali za kijamii

Wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa kukosekana kwa umeme kunarudusha nyuma maendeleo ya kitongoji kwani wanalazimika kufuata huduma zingine mahali palipo na umeme.

Sauti za wananchi.

Festo Manjechi ni Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mpwayungu amesema zaidi ya vitongoji 7 kati ya 10 vina uhitaji na nishati ya umeme, ameongeza kuwa mpaka sasa wamewasiliana na mamlaka husika juu ya uhitaji huo wa wananchi.

Sauti ya Festo Manjechi