Dodoma FM

Watoto wa zaidi ya miaka mitano wakatiwe tiketi wanapo safiri

6 November 2025, 1:44 pm

Sheria ya SUMATRA YA MWAKA 2020 inasema watoto wenye zaidi ya umri wa miaka mitano na kuendelea wana haki ya kupata tiketi kamili na siti zao maalum.Picha na youtube.com.

Baadhi ya abiria kuwa hukumbana na kero ya kuombwa wasaidie kubeba watoto pindi wanapo kuwa safarini kutokana na mzazi kukata siti moja huku watoto alio nao wakikosa mahali pa kukaa.

Na Anwary shaban.
Abiria wanao tumia huduma ya usafiri wa mabasi wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuwakatia tiketi watoto wanaozidi miaka mitano ili kuepuka usumbufu wakati wasafari.

Hayo yanajiri kutokana na malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya abiria kuwa hukumbana na kero ya kuombwa wasaidie kubeba watoto pindi wanapo kuwa safarini kutokana na mzazi kukata siti moja huku watoto alio nao wakikosa mahali pa kukaa.

Bi. Amina Omari, ni kondakta wa kampuni ya mabasi ya Championi yeye anasema tatizo hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara kutokana na ukosefu wa elimu kwa abiria kuhusu taratibu za usafiri.

Sauti ya Bi. Amina Omari,

Kwa upande wake Afisa kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Felichism Tarimo anasema kwa mujibu wa sheria ya usafiri kila abiria anapaswa kukaa kwenye siti yake vivyo hivyo hata kwa watoto wanao zidi miaka mitano wanapaswa kukaa kwenye siti .

Sauti ya Felichism Tarimo

Nao baadhi ya Abiria wamesema ni vyema wazazi kuwakatia siti watoto wakati wa safari ili kuondoa usumbufu kwa abiria wengine.

Sauti za abiria.

Kulingana na miongozo ya usafirishaji ya kampuni za mabasi na Sheria ya SUMATRA (Transport Licensing Regulations, 2020), watoto waliochini ya miaka 3–5 wanaweza kusafiri bila kulipia tiketi au kwa nusu tiketi, kulingana na sera ya kampuni, na watoto wenye zaidi ya umri wa miaka mitano na kuendelea wana haki ya kupata tiketi kamili na siti zao maalum.