Dodoma FM

Jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka mitatu

23 October 2025, 3:03 pm

Picha ni jengo la mahakama ya wilaya ya Kiteto.Picha na Kitana Hamis.

katika utetezi wake Mtumiwa huyo anasema anasingiziwa na baba wa mtoto huyo kwa kuwa anaugomvi nae.

Na Kitana Hamis.
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 20 alie fahamika kwa jina la Athuman Hatibu mkazi wa Laiseri Wilayani Kiteto amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka mitatu.

Kwamjibu wa Karimu Mushi amesema Mtumiwa huyo ametenda Kosa Kinyume na kifungo cha (130) kifungo kidogo cha Kwanza na chapili na kifungo cha (131) cha kununi ya Adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2023.

Maelezo ya Kosa nikwamba Mtumiwa alimdanganya Mtoto huyo aliye kuwa akicheza na Wezake na kumwita ili akamnunulie Pipi Dukani ndipo walipo fika Kichakani na kumbaka.
Tukio hili limetulazimu kufika ofisi za Ustawi wa jamii wilaya ya kiteto na kuongea na Afisa Ustawi pamoja na Mambo Mengine hapa wanasema wamefurahiswa na hukumu iliyo tolewa ili iwe fundisho kwa wengine.

Habari kamili.