Dodoma FM
Dodoma FM
9 October 2025, 5:17 pm

Picha ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu, wakati akifungua mafunzo kwa vikundi , katika ukumbi wa Nala Hotel, Jijini Dodoma. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Dkt. Kazungu amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza ujuzi na maarifa kwa wanavikundi ili waweze kuendesha miradi yao kwa tija na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku.
Na Lilian Leopold.
Mafunzo kupitia mfumo jumuishi wa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu yametajwa kuwa chachu muhimu ya kuboresha shughuli za kiuchumi kwa wanufaika wa vikundi hivyo.
Kauli hiyo imetolewa 08 Oktoba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu, wakati akifungua mafunzo kwa vikundi vilivyokidhi vigezo vya kupata mkopo wa asilimia 10, katika ukumbi wa Nala Hotel, Jijini Dodoma.
Dkt. Kazungu amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza ujuzi na maarifa kwa wanavikundi ili waweze kuendesha miradi yao kwa tija na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku.
Aidha, amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwa kujitokeza kwa wingi na kuonyesha dhamira ya dhati ya kuboresha maendeleo ya vikundi vyao.

Kwa upande wake, Meneja wa Tawi la LAPF, Bw. Honest Mushi, ameipongeza serikali kwa kuboresha mifumo ya utoaji wa mikopo, hatua iliyowezesha Benki ya CRDB kufikia halmashauri tano ikiwemo halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mafunzo hayo yameandaliwa na CRDB Foundation kwa lengo la kuwajengea wanavikundi uwezo katika masuala ya uendeshaji na usimamizi wa miradi pamoja na namna bora ya kukopa na kurejesha mikopo.