Dodoma FM
Dodoma FM
9 October 2025, 3:42 pm

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara yake katika eneo la Hombolo. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Aidha, amesema mradi huo ni wa mfano wa kuigwa nchini, na utawasaidia wakulima wengine kujifunza mbinu bora za kilimo cha zabibu na uchakataji wa bidhaa zake ili kuongeza thamani ya mazao yao.
Na Lilian Leopold.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amepongeza Jiji la Dodoma kwa ubunifu katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu uendelezaji wa zao la zabibu na uzalishaji wa mvinyo jijini humo.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika eneo la Hombolo, ambako kunapatikana kiwanda cha zabibu kinachomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mhe. Senyamule amempongeza Mkurugenzi wa Jiji pamoja na viongozi wa wilaya kwa kutekeleza mradi huo kwa ubunifu, akibainisha kuwa utachochea utalii wa kilimo na kuvutia wageni kuja kujifunza.
Aidha, amesema mradi huo ni wa mfano wa kuigwa nchini, na utawasaidia wakulima wengine kujifunza mbinu bora za kilimo cha zabibu na uchakataji wa bidhaa zake ili kuongeza thamani ya mazao yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Fredrick Sagamiko, amesema kwa sasa kiwanda hicho kipo kwenye hatua za mwisho za matengenezo na kipo mbioni kuanza uzalishaji.
Ameongeza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho kulileta changamoto kwa wakulima wa eneo la Hombolo ambao ni wazalishaji wakubwa wa zabibu, hivyo kufunguliwa kwake upya kutasaidia kutatua changamoto ya masoko na kuongeza kipato kwa wakulima.