Dodoma FM

Odilo yaishukuru DMG kwa udhamini baada ya kung’ara ligi ya kikapu

8 October 2025, 5:21 pm

Picha ni wachezaji wa timu ya kikapu ya Odilo kutoka mkoa wa Dodoma. Picha na Hamis Makila.

Wachezaji hao wameipongeza kampuni hiyo kwa kujitokeza kuunga mkono michezo mkoani Dodoma na wameomba kuendelea kudhaminiwa katika mashindano yajayo.

Na Hamis Makila.

Baada ya kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dodoma kwa msimu wa 2025, timu ya kikapu ya Odilo imeishukuru kampuni ya Dodoma Media Group (DMG) kwa udhamini wa jezi walizozitumia katika michuano hiyo.

Wakizungumza na Dodoma FM , baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wamesema kuwa michuano ilikuwa na ushindani mkubwa, lakini udhamini wa DMG uliwapa hamasa na kuimarisha ari ya ushindani.

Aidha, wachezaji hao wameipongeza kampuni hiyo kwa kujitokeza kuunga mkono michezo mkoani Dodoma na wameomba kuendelea kudhaminiwa katika mashindano yajayo.

Sauti za wachezaji.

Kwa upande mwingine, ligi hiyo kwa sasa ipo katika hatua ya fainali, ambapo Dom Spurs watamenyana na Don Bosco Panthers katika michezo mitano ya kuwania ubingwa wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dodoma kwa upande wa wanaume. Timu itakayoshinda michezo mitatu kati ya mitano itajinyakulia taji la ubingwa wa msimu huu.