Dodoma FM

Wananchi Mzula, Chikanga waomba shule ya sekondari

8 October 2025, 12:37 pm

Wamesema kuwa changamoto hiyo imekuwa hatari kwa wanafunzi hususani wa kike kwani wamekuwa wakikumbana na vishawishi mbalimbali vinavyo pelekea kupata ujauzito. Picha na Google.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Muungano Matonya Mtukamsihi     amesema zimekuwepo hatua za wananchi kuanzisha ujenzi wa shule ya sekondari lakini hazijafanikiwa kukamilika.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa vitongoji Mzula na Chikanga Kata ya Muungano Wilaya ya Chamwino wameiomba serikali kutimiza azima ya wazazi juu ya ujenzi wa shule ya sekondari kutokana na shule iliyopo kuwa umbali mrefu.

Wamesema kuwa changamoto hiyo imekuwa hatari kwa wanafunzi hususani wa kike kwani wamekuwa wakikumbana na vishawishi mbalimbali vinavyo pelekea kupata ujauzito.

Aidha wameongeza kuwa kupitia juhudi za wananchi wamekuwa na kiu ya kujenga sekondari yao lakini wamekosa nguvu ya kukamirisha ujenzi huo

Sauti za wananchi.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Muungano Matonya Mtukamsihi   amesema zimekuwepo hatua za wananchi kuanzisha ujenzi wa shule ya sekondari lakini hazijafanikiwa kukamilika.

Mtukamsihi ameongeza kuwa licha ya wazazi kuhamasika kupeleka watoto shule lakini kukosekana kwa sekondari baadhi ya watoto wameshindwa kuhitimu masomo yao.

Sauti ya Matonya Mtukamsihi.

Serikali ya Tanzania imeendelea kuonyesha jitihada kubwa za kujenga shule na madarasa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa kuboresha upatikanaji na ubora wa elimu.