Dodoma FM
Dodoma FM
6 October 2025, 6:03 pm

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika hafla ya Capital City Marathon . Picha na Lilian Leopold.
Amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mtu kujitokeza kushiriki katika shughuli za michezo ili kudumisha afya na kuongeza ubunifu katika maisha ya kila siku.
Na Lilian Leopold.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara na kijamii zinazojitokeza kupitia shughuli za michezo kama mbio za Capital City Marathon zilizofanyika Oktoba 5, 2025 katika ukumbi wa Chimwaga.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Senyamule amesema kushiriki michezo ni sehemu muhimu ya kujenga afya bora na kuimarisha mahusiano baina ya watu, jambo linaloweza kuleta maendeleo kwa jamii.
Amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mtu kujitokeza kushiriki katika shughuli za michezo ili kudumisha afya na kuongeza ubunifu katika maisha ya kila siku.
Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa kupitia matukio kama haya, wananchi wanapata nafasi ya kujenga urafiki, kubadilishana mawazo na kuibua mitazamo mipya ya kimaendeleo, hasa katika sekta ya biashara ndani ya Jiji la Dodoma.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Alhaji Jabir Shekimweri amewapongeza waliopata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Dodoma, ikiwemo mradi wa reli ya kisasa (SGR) na uwanja wa ndege wa Dodoma.