Dodoma FM
Dodoma FM
6 October 2025, 11:43 am

Aidha, amesema changamoto kubwa kwa vijana wengi wa sasa ni kutegemea wazazi wao badala ya kujituma na kupambana kwa ajili ya maisha yao, hali inayowadumaza kimaendeleo. Picha na Blog.
Muhuri amesema ukosefu wa kipato umesababisha baadhi ya wasichana kujiingiza kwenye mahusiano yasiyo rasmi, jambo linalopelekea wengine kupata mimba za utotoni na hatimaye kutelekezwa.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa baadhi ya vijana kushindwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji ni miongoni mwa sababu zinazowafanya kushindwa kulea familia zao na kujiingiza katika makundi yasiyofaa.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Msamalo, Bi. Ngw’ashi Muhuri, amesema changamoto ya vijana wengi kukaa mitaani bila kufanya kazi imepelekea wengi wao kushindwa kuhimili mahitaji ya familia, hali inayochochea umasikini na migogoro ya kifamilia.
Muhuri amesema ukosefu wa kipato umesababisha baadhi ya wasichana kujiingiza kwenye mahusiano yasiyo rasmi, jambo linalopelekea wengine kupata mimba za utotoni na hatimaye kutelekezwa.
Aidha, amesema changamoto kubwa kwa vijana wengi wa sasa ni kutegemea wazazi wao badala ya kujituma na kupambana kwa ajili ya maisha yao, hali inayowadumaza kimaendeleo.
Kwa upande wao, baadhi ya vijana wameeleza kuwa kubweteka majumbani ni chanzo cha kukosa maarifa ya kujitegemea na kuwafanya wengi kuona maisha ni magumu.
Wameongeza kuwa ni muhimu kwa vijana kutambua nafasi zao katika kujitafutia maisha na kuanzisha vyanzo halali vya kipato badala ya kujihusisha na makundi yasiyofaa.