Dodoma FM

Pambano la ngumi kuanza rasmi Oktoba 18

2 October 2025, 4:23 pm

Picha ni baadhi ya mabondia watakaoshiriki katika Kibaigwa vitasa mitano tena. Picha na Hamis Makila.

Kwa mujibu wa mratibu, mabondia mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya mkoa wa Dodoma na nje yake wamethibitisha kushiriki.

Na Hamis Makila.

Kuelekea pambano la ngumi litakalofanyika Kibaigwa, mratibu wa pambano hilo ameeleza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na mashabiki wanatarajiwa kushuhudia burudani ya kipekee.

Pambano hilo limepangwa kufanyika kuanzia tarehe 18 Oktoba katika uwanja wa Amani Kibaigwa, likiwa na lengo kuu la kuibua na kukuza vipaji vya vijana wanaojitokeza katika mchezo wa ngumi.

Sauti ya Hamis Makila.