Dodoma FM
Dodoma FM
2 October 2025, 3:42 pm

Mikopo hiyo inawapa faida zaidi ikilinganishwa na mikopo mingine ya mtaani ambayo mara nyingi ina riba kubwa.
Na VictorChigwada.
Vijana wa Kata ya Msamalo, Wilaya ya Chamwino, wameipongeza serikali kwa kujali kundi la vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu kwa kuendelea kutoa mikopo ya asilimia kumi.
Wakizungumza na Taswira ya Habari, baadhi ya vijana wamesema kuwa mikopo hiyo imekuwa ikisadia vijana wengi kuamka kifikra na kuanzisha miradi mbalimbali inayotoa ajira na kipato.
Wameongeza kuwa mikopo hiyo inawapa faida zaidi ikilinganishwa na mikopo mingine ya mtaani ambayo mara nyingi ina riba kubwa.
Aidha, wamewaomba vijana wenzao kujiunga katika vikundi mbalimbali ili kunufaika na mikopo hiyo, sambamba na kuhakikisha wanafanya marejeshokwa wakati sahihi ili wengine pia waweze kunufaika na mikopo isiyo na riba.
Kwa mujibu wa mwongozo wa Serikali, kila halmashauri inalazimika kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wanawake (4%), vijana (4%), na watu wenye ulemavu (2%).