Dodoma FM

Wakazi Mjelo waomba suluhisho la kisima cha maji

2 October 2025, 11:05 am

Hali hiyo inatokea zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa mradi mkubwa wa kisima cha maji, ambao ulitarajiwa kumaliza tatizo la uhaba wa maji safi na salama katika vijiji vya kata hiyo. Picha na RUWASA.

Wameeleza kuwa hali hii imeendelea kuwatesa wananchi, ambao bado wanategemea maji yasiyo safi kutoka visima vya makorongo.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa Kijiji cha Mjelo, Kata ya Handali, Wilaya ya Chamwino, wameitaka Serikali kushughulikia changamoto zinazohusiana na mkandarasi wa kisima cha maji, ili kuondoa adha wanayokabiliwa nayo wananchi.

Hali hiyo inatokea zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa mradi mkubwa wa kisima cha maji, ambao ulitarajiwa kumaliza tatizo la uhaba wa maji safi na salama katika vijiji vya Kata hiyo. Wameeleza kuwa hali hii imeendelea kuwatesa wananchi, ambao bado wanategemea maji yasiyo safi kutoka visima vya makorongo.

Sauti za wananchi.

Emmanueli Tanaga, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mjelo, amesema kuwa mkandarasi wa kwanza aliyetarajiwa kukamilisha mradi huo alishindwa, na mkandarasi mpya aliyepewa kazi bado anakabiliwa na changamoto katika kukamilisha mradi kwa haraka.

Sauti ya Emmanuel Tanaga.

Tanaga ameongeza kuwa licha ya kukamilika kwa ujenzi wa tenki, bado kuna changamoto ya upungufu wa fedha zinazohitajika kuendelea na ukamilishaji wa mradi huo.

Sauti ya Emmanuel Tanaga.