Dodoma FM
Dodoma FM
1 October 2025, 4:53 pm

Miundombinu ya maji kuharibika mara kwa mara hasa mabomba kupasuka, hali inayosababisha visima na vituo vya maji kushindwa kutoa huduma ya uhakika. Picha na RUWASA.
Wananchi hao wamesema kuwa hapo awali baadhi ya visima vilisimamiwa na kamati za huduma ya maji vijijini, na wakati huo hakukuwa na changamoto kubwa, hasa kwenye miundombinu ya maji.
Na Victor Chigwada.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Chamwino wameiomba Mamlaka ya Usimamizi wa Maji Vijijini (RUWASA) kuongeza nguvu katika kusimamia miundombinu ya maji vijijini, kwani wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama.
Wananchi hao wamesema kuwa hapo awali baadhi ya visima vilisimamiwa na kamati za huduma ya maji vijijini, na wakati huo hakukuwa na changamoto kubwa, hasa kwenye miundombinu ya maji.
Hata hivyo, kwa sasa kumekuwa na changamoto kubwa ya miundombinu, ikiwemo mabomba kupasuka mara kwa mara, jambo linalosababisha vituo vya maji kushindwa kutoa huduma ipasavyo.
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Chamwino, Iddi Magoti, amesema kuwa mfumo wa kusimamia visima vya maji kutoka kwa wananchi na kuingia RUWASA ni matokeo ya mabadiliko ya Sheria ya Maji ya mwaka 2019.
Aidha, Magoti amebainisha kuwa pamoja na mabadiliko hayo, muundo wa usimamizi wa maji bado unajumuisha wananchi wa eneo husika, ambao wanaendelea kushiriki katika usimamizi wa visima na kuhakikisha huduma ya maji inafika kwa jamii.
Sheria ya Maji ya 2019 ilibadilisha mfumo wa usimamizi kutoka mikononi mwa kamati za maji vijijini na kuanzisha RUWASA kama chombo cha kitaifa chenye mamlaka ya kusimamia huduma hizo.