Dodoma FM

Wajibu wa wazazi, walezi katika elimu ya afya ya uzazi kwa vijana

25 September 2025, 3:06 pm

Wasichana hasa wasichana balehe wanapaswa kupatiwa elimu bora ya afya ya uzazi ili waweze kujitambua . Picha na UN news.

Mikakati kama vile elimu ya kina ya afya ya uzazi kwa vijana, upatikanaji wa huduma rafiki za afya, na ushirikishwaji wa jamii katika kubadili mitazamo potofu kuhusu mimba za utotoni inahitajika.​

Na Mariam Matundu.

Wazazi na walezi wana wajibu wa kuhakikisha vijana wanapata elimu ya Afya ya uzazi ili waweze kujitambua na kuepukana na madhara mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni .

Kwa mujibu wa WHO Kwa mwaka 2021, inakadiriwa msichana 1 kati ya 25 alijifungua kabla ya umri wa miaka 20, ikilinganishwa na 1 kati ya 15 miongo miwili iliyopita. Hata hivyo bado kuna tofauti kubwa. Katika baadhi ya nchi, karibu msichana 1 kati ya 10 (mwenye umri wa miaka 15-19) hujifungua kila mwaka.