Dodoma FM

Wafanyakazi wa nyumbani wanakumbana na ukatili-ILO

23 September 2025, 4:46 pm

zaidi ya watu milioni moja wameajiriwa kama wafanyakazi wa nyumbani nchini.Picha na UN news.

Wafanyakazi wa nyumbani bado wanakumbwa na unyanyasaji kwa sababu kazi hiyo haieshimiwi kama kazi rasmi.

Na Lilian Leopold.
Kulingana na ripoti kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), zaidi ya watu milioni moja wameajiriwa kama wafanyakazi wa nyumbani nchini na wengi wao wanakumbwa na ukatili wa kimwili na wa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kutolipwa stahiki zao.

Angela Benedicto ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Wote Sawa, amesema kuwa wafanyakazi wa nyumbani bado wanakumbwa na unyanyasaji kwa sababu kazi hiyo haieshimiwi kama kazi rasmi na badala yake, inaonekana kama kazi ya msaada tu, jambo linalowanyima wafanyakazi hawa haki zao za msingi.

Aidha, Angela amepongeza hatua ya serikali kuonyesha nia ya kuridhia Mkataba wa Kimataifa namba 189 wa ILO, ambao ukipitishwa, utakuwa msaada mkubwa katika kuhakikisha heshima, ulinzi na haki kwa wafanyakazi wa nyumbani wanaochangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa.

Sauti ya Angela Benedicto .