Dodoma FM

Weledi, maadili nyenzo muhimu ulinzi wa mwandishi wa habari

20 September 2025, 9:47 am

Picha ni mkutano uliowakutanisha wadau wa Habari ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ,Takukuru,maafisa wa serikali,maafisa Habari wa serikali na waandishi wa Habari jijini Dodoma.Picha na MCT.

Baraza la Habari Tanzania MCT September 18 mwakahuu 2025 limewakutanisha wadauwa Habari kwa lengo la kujenga uhusiano mzuri kwa taasisi za serikali na waandishi wa Habari ili kuwezesha kazi ya wanahabari katika kuhabarisha umma pamoja na kujadili masuala ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari.

Na Mariam Matundu.
Weledi na Maadili vimetajwa kuwa nyenzo muhimu katika ulinzi na usalama wa mwandishi wa Habari hapa nchini wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kitaaluma.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau wa Habari ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ,Takukuru,maafisa wa serikali,maafisa Habari wa serikali na waandishi wa Habari katibu mtendaji wa baraza la Habari Tanzania MCT Ernest Sungura amesema iwapo waandishi wa Habari wataandika Habari za ukweli watajikinga na madhira mabalimbali.

Sauti ya Ernest Sungura.

Amesema katika kipindi cha uchaguzi wanahabari wana mchango mkubwa kuhabarisha umma taarifa muhimu na hivyo ni muhimu kuzingatia uadilifu ili kutimiza adhima hiyo.

Sauti ya Ernest Sungura.

Nae mwakilishi wa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini halmashauri ya jiji la Dodoma Denis Gondwe amepongeza baraza la Habari kuandaa mkutano huo na hasa katika kuelimisha kuhusu sheria ya upatikanaji wa taarifa.

Sauti ya Denis Gondwe .