Dodoma FM

Elimu ya haki za watoto wasaidia kukabiliana na ukatili wa kijinsia

18 September 2025, 4:49 pm

Picha ni katika Mkutano wa pili wa Jukwaa la msichana cafe uliofanyika jijini Dodoma.Picha na Seleman Kodima.

Ikumbukwe kwa jukwaa la msichana cafe limewakutanisha wawakilishi kutoka mikoa minne ambayo ni Dar es salaam,Dodoma,Pwani na Tabora ambapo lengo kuu  ni kujadili changamoto wanazokutanazo wawakilishi hao.

Na Seleman Kodima.

Utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu haki za mtoto wa kike  imetajwa kuleta mwangaza mpya kwa jamii katika kulinda na kumtetea mtoto huyo katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Aidha Vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya mtoto vimetajwa kupungua katika baadhi ya maeneo hapa nchini.

Akizungumzia Mafanikio hayo Mkurugenzi  mteule wa shirika la Msichana Initiative, Consolata Chikoti wakati wa Mkutano wa pili wa Jukwaa la msichana cafe uliofanyika jijini Dodoma ambapo amesema jamii wameendelea kuunga mkono mapambano hayo na hatimaye wameona hadithi za mafanikio ya kweli kumtetea mtoto wa kike.

Bi Consolata amesema kwa mwaka huu pekee Jukwaa hilo limepokea kesi 104 ambapo 13 zikiwa za ndoa za utotoni,36 mimba za utotoni,55 ukatili mwingine kwa mtoto.

Sauti ya Bi Consolata.
Picha ni katika Mkutano wa pili wa Jukwaa la msichana cafe uliofanyika jijini Dodoma.Picha na Seleman Kodima.

Aidha amesema lengo la kuwakutanisha wawakilisha wa Majukwaa hayo ni kutambua mchango wao wa kuifikia jamii na kuibua masuala ya jinsia.

Sauti ya Bi Consolata.

Kwa upande wao wawakilishi wa jukwaa hilo kutoka Mikoa ya Tabora na Dodoma wamesema kuwa upo mchango wa jukwaa hilo kwenye kupunguza vitendo vinavyomkwamisha mtoto wa kike kufikia ustawi wake.

Sauti za wawakilishi.

Ikumbukwe kwa jukwaa la msichana cafe limewakutanisha wawakilishi kutoka mikoa minne ambayo ni Dar es salaam,Dodoma,Pwani na Tabora ambapo lengo kuu  ni kujadili changamoto wanazokutanazo wawakilishi hao na kujua namna wanavyoweza kuwa sehemu ya utatuzi  wa changamoto hizo Hususani Matukio ya ukatili wa kijinsia,Mimba za Utotoni,Ndoa za Utotoni na Kuhakikisha usalama wa mtoto unapewa kipaumbele katika jamii.