Dodoma FM
Dodoma FM
10 September 2025, 3:44 pm

Afisa Ustawi wa Jami jiji la Dodoma Rosemary Nicodemus wakati akizungumza na Taswira ya Habari anasema uwepo wa migogoro katika familia ni jambo linaloathiri zoezi la unyonyeshaji kwa mama.
Na Lilian Leopold.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeeleza kuwa moja ya mikakati yake katika kuimarisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ni kusuluhisha migogoro ya kifamilia ili kuhakikisha mama wanapewa mazingira salama na yenye msaada wakiendelea kunyonyesha.
Suala la unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni muhimu kwa kuhakikisha ustawi bora wa mtoto ambapo kwa mujibu wa wataalamu wa afya wanasema suala hilo linapaswa kufanyika kwa ufanisi.