Dodoma FM

Zoezi la chanjo ya mifugo lazinduliwa Mbalawala Dodoma

3 September 2025, 5:26 pm

Picha ni Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Gratian Mwesiga wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa kwa mgeni rasmi aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.Picha na Jiji la Dodoma.

Uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Nchini Tanzania ulifanyika tarehe 16 Juni 2025 katika Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi, Mkoa wa Simiyu, katika hafla hiyo, Rais Samia alizindua rasmi kampeni ya kitaifa ya chanjo ya mifugo na utambuzi wa wanyama, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha afya ya mifugo na kufungua masoko ya kimataifa.

Na Lilian Leopold.
Zoezi la Uzinduzi wa chanjo na utambuzi wa mifugo linalofanyika nchi nzima limezinduliwa katika Kata ya Mbalawala jijini Dodoma kwa lengo la kutoa chanjo kwa ng’ombe, mbuzi na kondoo ili kuwaepusha na ugonjwa wa homa ya mapafu na sotoka.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Gratian Mwesiga wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa kwa mgeni rasmi aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, amesema kuwa serikali imetoa chanjo mbalimbali kwaajili ya kuhakikisha mifugo inakuwa salama.
Aidha, ameeleza kuwa serikali imeanzisha rasmi utambuzi wa mifugo kwa njia ya kielektroniki hatua ambayo inatarajiwa kurahisisha utunzaji, usalama na uuzaji wa mifugo.

Sauti ya Gratian Mwesiga.

Kwa uapnde wake, Afisa Tarafa Kata ya Zuzu, Ibrahim Ally amewapongeza wafugaji kwa jitihada zao za kuzalisha bidhaa bora zinazotokana na mifugo na kuwasisitiza umuhimu wa kuchanja na kutambua mifugo yao.

Naye, Mwakilishi kutoka Wizara ya Mifugo na Kaimu Afisa Mfawidhi Kituo cha Huduma za Mifugo Kanda ya Kati (ZVC), Dkt. Deoniz Ibrahim amefafanua kuwa wanatarajia kuchanja takribani mifugo milioni kumi.

Sauti ya Dkt. Deoniz Ibrahim