Dodoma FM

Vinara wa uwajibikaji wachaguliwa Inzomvu

22 August 2025, 4:06 pm

Picha ni wakazi wa kijiji cha Inzomvu wilayani Mpwampwa wakiunga mkono uwepo wa vinara wa uwajibikaji. Picha na Seleman Kodima.

Baadhi ya Vinara wa Uwajibikaji na usimamizi wa Rasilimali za umma kupitia Mradi wa Raia Makini waliochanguliwa na wananchi wameahidi kutumika vyema kwa maslahi pana ya jamii yao.

Na Seleman Kodima.

Wakazi wa kijiji cha Inzomvu wilayani Mpwapwa wameonesha kuunga mkono hatua ya uwepo wa Vinara wa uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali ambao wametoka ndani ya kijiji hicho.

Uungwaji mkono huo umetokea wakati wa upigaji wa kura za kuwachagua Vinara hao ambapo zoezi hilo liliratibiwa na viongozi wa serikali ya kijiji kwa kushirikiana na mratibu wa shirika la Wajibika John Mwilongo.

Akizungumza katika zoezi hilo,Afisa Mtendaji wa kijiji Inzomvu Ester Mgoba amesema hatua ya kupatikana kwa vinara hao itasadia kuongeza hali ya uwajibikaji katika mradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mratibu wa Wajibika John Mwilongo amesema hatua ya kupatikana kwa Vinara hao ni muhimu katika kufikia lengo la kuwajengea uwezo na hatimaye kuanza majukumu yao.
Baadhi ya Vinara wa Uwajibikaji na usimamizi wa Rasilimali za umma kupitia Mradi wa Raia Makini waliochanguliwa na wananchi wameahidi kutumika vyema kwa maslahi pana ya jamii yao.