Dodoma FM
Dodoma FM
22 August 2025, 3:45 pm

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kimagai wakiwa pamoja na Vinara wa uwajibikaji kupitia Mradi wa Raia Makini. Picha na Seleman Kodima.
Mradi huu unatekelezwa katika mikoa 5 nchini Tanzania ambapo mkoani Dodoma unatekelezwa katika wilayani Mbili ambazo ni Bahi na Mpwapwa .
Na Seleman Kodima.
Katika kuhakikisha jamii inakuwa na uwezo wa kusimamia na kufanya ufatiliaji wa Rasilimali za umma ,Kijiji cha Kimagai wilayani Mpwapwa kimefanikiwa kupata vinara wa masuala ya uwajibikaji kupitia Mradi wa Raia
Hatua hiyo ni utekelezaji wa kuhakikisha jamii wanakuwa na uwezo wa kufatilia na kusimamia miradi ya maendeleo kama lilivyo lengo la mradi huo Kukuza ushiriki wa wananchi katika Uwajibikaji na Usimamizi wa Rasilimali za Umma.
Akiutambulisha Mradi huo kwa Wananchi wa kijiji hicho,Mratibu wa Shirika la Wajibika John Mwilongo amesema Kuwezesha kamati za wanajamii kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika vijiji vyao.
Aidha amesema zipo sifa ambazo mwanajamii anatakiwa kuwa nazo hili kuwa sehemu ya Vinara Raia makini ikiwa ni pamoja na awe na umri wa miaka 18 hadi 45,awe anajua kusoma na kuandika na kujieleza,awe sio kiongozi wa serikali ya mtaa lakini amekuwa akichangia miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bahati Magumula ametoa wito kwa wananchi wa kijiji hicho kushiriki vyema katika nafasi hizo ili kusaidia kusukuma guruduma la maendeleo katika eneo hilo.

Pamoja na hayo katika zoezi hilo Vinara wa Raia makini walifanikiwa kuchaguliwa katika mkutano wa kijiji kwa uwino wa wanaume ,wanawake na watu wenye Ulemavu.
Mradi huu unatekelezwa katika mikoa 5 nchini Tanzania ambapo mkoani Dodoma unatekelezwa katika wilayani Mbili ambazo ni Bahi na Mpwapwa .
Aidha Shirika lisilo la Kiserika la WAJIBIKA wanatekeleza mradi huu chini ya Mwamvuli wa mashirika ya WAJIBU – Institute of Public Accountability na Policy Forum kwa lengo la kukuza ushiriki wa wananchi katika uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za umma kwa maendeleo endelevu Tanzania.