Dodoma FM
Dodoma FM
19 August 2025, 3:38 pm

Kwa mujibu wa ripoti ya Mahakama Kuu na kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma, mashauri ya mirathi yanagusa uchumi mkubwa wa mtu mmojammoja na wa taifa kwa ujumla.
Na Joseph Julius.
Wito umetolewa kwa wadau wa sheria kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu taratibu sahihi za mirathi ili kuhakikisha haki inapatikana.
Wito huo umetolewa na Mwanasheria HAROD AMOS MALIMA wakati akizungumzia umuhimu wa jamii kufahamu taratibu na sheria za mirathi.
Aidha ameto ufafanuzi wa kina kuhusu taratibu na sheria zinazohusu masuala ya mirathi nchini Tanzania, akibainisha umuhimu wa wananchi kufahamu haki zao ili kuepuka migogoro ya kifamilia.