Dodoma FM

Mpango wa 95 tatu utafanikiwa kwa wananchi kupima afya

19 August 2025, 2:50 pm

Vijana wenye VVU wanaendelea kuhimizwa kuzingatia matumizi ya Dawa na Jamii kuwa karibu nao.Picha na Google.

Ni bonanza lililohusisha vijana wenye umri wa miaka 10–19, ambapo wameshiriki katika majadiliano ya wazi na yenye mwongozo kuhusu ufuatiliaji wa matibabu , huduma bora za kliniki, mahusiano na marafiki, na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyapaa.

Na Seleman Kodima.

Ili kufanikisha Mpango wa 95, tatu za kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU, wananchi wametakiwa kuendelea kujitokeza kupima afya zao ili kufahamu hatua zipi wachukue pindi wanapokutwa VVU ili wawe Salama.

Hatua hii inajiri ikiwa wa ripoti za Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI, ikibainisha kuwa asilimia 57 pekee ya watoto wenye umri wa miaka 0–14 wanaoishi na VVU duniani wanaopata tiba, ikilinganishwa na asilimia 77 ya watu wazima.

Aidha ripoti hiyo inaeleza kuwa Kusini mwa Jangwa la Sahara – ambako zaidi ya watoto milioni 1.3 wanaishi na VVU – upatikanaji wa huduma za tiba bado ni mdogo.
Aidha hapa nchini takribani watoto 6,500 chini ya miaka 15 huambukizwa VVU kila mwaka, hali inayoonesha hitaji la mbinu bunifu na rafiki kwa vijana, zinazoshughulikia mahitaji ya kiafya na kisaikolojia kwa pamoja.

Katika Kufanikisha hatua madhubuti za kuwaleta pamoja Vijan,Taasisi ya AIDS Healthcare Foundation (AHF) kwa kushirikiana na Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) wamewakutanisha pamoja vijana na watoto kupitia Bonanza Maalum huku likichangiza kutoa elimu na kuwapa nafasi kuadhimisha Siku ya Vijana Dunia kwa Michezo mbalimbali.

Akizungumza baada ya Kufungua Bonanza hilo,Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Yohana Magembe kutoka Hospitali ya Makole amesema kuwa hatua ya kuwakutanisha Vijana hao ni sehemu ya kufanikisha mpango wa 95 tatu ambapo jamii inatakiwa kuendelea kujitokeza ili kufahamu afya zao.

Sauti ya Dkt Yohana Magembe.

Kwa upande wake meneja Kanda Haika Mtui amesema ipo haja ya kuendelea kutoa ushirikiano ili kufanikisha mapango huo,na kutaka hatua zaidi kuwekwa katika kinga ili kupunguza gharama za mapambano hayo.

Sauti ya Haika Mtui .

Nae Mwakilishi wa Meneja Mradi wa EGPAF-Dodoma Dkt Monica Peter amesisitiza vijana kujitokeza kupata Huduma rafiki katika Vituo vya afya ili kujua hali zao za kiafya.

Sauti ya Dkt Monica Peter.

Baadhi ya Vijana Waelimishaji Rika Walioshiriki katika Tukio hilo,Daniel Gabriel na Agnes William wametoa wito kwa Vijana wenye VVU kuzingatia matumizi ya Dawa na Jamii kuwa karibu nao ili kuwa na jamii yenye Usawa bila unyanyapa.

Sauti za Daniel Gabriel na Agnes William