Dodoma FM
Dodoma FM
18 August 2025, 5:17 pm

Aidha, wananchi walielezwa kuhusu miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na UCSAF ikiwemo maendeleo ya ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano nchini.
Na Mariam Kasawa.
Imeelezwa kuwa mawasiliano ni muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa hili hasa katika shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji.
Hayo yamesemwa na mkuu wa kanda ya kaskazini wa mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF ambapo amesema wana wajibu wa kuhakikisha mawasiliano yanafika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini na maeneo ambayo yana huduma hafifu za kimtandao.
Aidha amewataka wananchi kufika katika ofisi zao ambazo zipo maeneo mbalimbali ikiwemo hapa mkoani Dodoma ambao wanakabiliwa na changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao ili waweze kusaidiwa.
Kwa kushiriki maonesho ya Nane Nane, UCSAF inaendeleza dhamira yake ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kunufaika na mawasiliano bora kama chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.