Dodoma FM
Dodoma FM
4 August 2025, 5:42 pm

Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1-7 Agasti
Na LovenesMiriam.
Imeelezwa kuwa ushirikishaji wa wanaume katika suala la unyonyeshaji kwa mama ni muhimu ili kuhakikisha afya ya mama na mtoto.
Hayo yamebainishwa na Bi Neema Joshua Mkurugenzi msaidizi wa huduma za lishe kutoka wizara ya afya katika viwanja vya St.johm Dodoma ikiwa ni moja ya shuhuli zinazofanyika kutoa elimu kwa jamii ya wiki ya unyonyeshaji kupitia ligi ya mpira.
Bi Neema amesema kuwa wanaume wanapaswa kuwa na mtazamo na kuthamini unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
Aidha Bi Neema amesema kuwa maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto hasa ni kipindi anapozaliwa mtoto hawezi kula chakula kingine zaidi ya maziwa ya mama ambayo yana virutubisho vyote muhimu.
Katika hatua nyingine jamii imeshauriwa kuzingatia unyonyeshaji wa maziwa ya mama na kumsaidia mama kazi ili kupata muda wa kunyonyesha.

Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1-7 Agasti huku kauli mbiu kwa mwaka huu ikiwa ‘’thamini unyonyeshaji,weka mazingira kwa mama na mtoto’’ ikienda sambamba na shughuli mbalimbali za kitaifa,kijamii na kijimbo katika kufikisha elimu ya unyonyeshaji kwa wananchi.